kumpeleka uk katika mji wa Harrow north west london.Kwa makubaliano ya kwamba atamlipa pound 50kwa mwezi ambayo ni sawa na 120,000sh za kitanzania ambayo atakuwa anaituma direct kwa mwanae anaesoma chuo ili alipie ada.
ila huyo bosi wake alibadilika kazi haikwenda kama walivyoelewana akawa anafanyishwa kazi masaa 20 kwa siku bila mapumziko,bila malipo na alimnyang'anya passport yake ili asimkimbie huyo mwajiri wake.Mwanahamisi alikuwa akishindia slace za mikate miwili siku nzima na akinyimwa chakula na huyo mwajiri wake.
SEEDA KHAN MWAJIRI WA MWANAHAMISI.
Mwanahamisi alikuwa akilala jikoni, ndani ya miaka mitatu na huyu mama aliweka kengele alalapo mwanahamisi akipiga tu anamka na kwenda kumuudumia,mwanahamisi wazazi wake walifariki alikataliwa na mwajiri wake kwenda tanzania kwenye mazishi na binti yake aliolewa bila yeye kuudhuria.
Mwanahamisi alibahatika kumriport mwajiri wake na alifunguliwa kesi na mwanahamisi ameshinda ,mwajiri wake atamlipa pound 25,000 na atafungwa miezi 9 nakupigwa faini ya pound 15000 kwa selikali.
MWANAHAMISI MRUKE